pakua-mixtape-5-kali-za-taarab-kwenye-mdundo-(mp3-download)

Pakua Mixtape 5 kali za Taarab Kwenye Mdundo (MP3 Download)

Muziki wa Taarab Tanzania ni miongoni mwa kigezo kikubwa katika kuuza mziki wa nchi hiyo.

Pakua Mixtape 5 kali za Taarab Kwenye Mdundo

Hivyo, katika kuipa hadhi mziki wa taarab tumekuandalia orodha ya mixtape tano kali za taarab kwa mashabiki wa muziki huo.

Taarab Mdundo Mix #01

Huu ni mchanganyiko wa mziki kutoka kwa Isha Masahuzi, Leyla Rashid na Jahazi Unique Taarab.

Hizi ni nyimbo zinazoangazia umuhimu wa upendo.

Taarab Mdundo Kabambe #06

Huu ni mchanganyiko wa muziki mpya wa Taarab. Moja wapo ya nyimb kali kwenye mixtape hii ni Mauzauza ilioachiwa na Zuchu akimshirikisha mamake Bi. Khadija Kopa.

Wasanii wengine husika kwenye mix hii ni kama vile Jahazi Unique, Khadija Yusuf na Zuhura Shaabani.

Taarab Mdundo Mix #07

Hizi ni nyimbo za michambo ambapo ni mchanganyiko kutoka kwa wasanii kama vile Leila Rashid, Khadija Kopa na Diamond Platnumz.

Nyimbo hizi zina maudhui ya michambo kwa wale wanaopenda kujihusisha na yasiyowahusu.

Taarab Mdundo Safi #05 Mix

Mixtape hii ina mchanganyiko ya nyimbo za wasanii tajika Tanzania kama vile; Mbosso, Lava Lava,Diamond Platnumz na Yamoto band.

Mixtape hii ni bora kwa wale wanaotaka kujifurahisha baada ya kuwa na siku mrefu.

Taarab Mdundo Mix #02

Huu ni mchanganyiko wa taarab tupu kutoka kwa waimbaji marufu wa taarab wakiwemo; Jahazi Fatuma, Jahazi Unique Taarab na Isha Mashauzi.

Pakua mix hii upate kujifunza mengi kutoka kwa waimbaji hawa wenye mafunzo mbalimbali.

Share